Vikosi vya Umoja wa Mataifa vikilinda amani DRC

Kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.

Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimearifu kuwa Padri Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini na ndipo wakati mtu mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.

Tukio hilo lilijiri wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.

Taarifa zinadai kuwa muuaji huyo ni kutoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji