Arsene Wenger

Baada ya Arsenal jana kuitandika AC Millan, kwa mabao 3-, uwenda mashabiki wa Arsenal wanaweza kutuliza mzuka wa kumlazimisha Mzee wenga kung’atuka kwenye timu ya Arsenal.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Danny Welbeck ambaye alifunga magoli mawili na goli la tatu lilifungwa na Danny Welbeck huku goli la AC Millan lilifungwa na Hakan Calhanoglu

Kwa matokeo hayo inaifanya Arsenal ivuke kwenye hatua nyingine kwa jumla ya magoli 5-1  Ukijumuisha na yale magoli mawili waliyoyapata ugenini.

Danny Welbeck

Licha ya Arsenal kutulizwa hasira lakini kwa upande wake Mzee Wenger yeye anaofia kukutana na Atletico Madrid hatua inayofuata.

Atletico Madrid wamekuwa wakicheza vizuri na walifika robofainali Europa League baada ya kuwalaza Lokomotiv Moscow 5-1 mechi ya marudiano.

Nyota wa zamani wa Liverpool na Chelsea Fernando Torres alifunga mabao mawili nao Angel Correa, Saul Niguez na Antoine Griezmann wakafunga moja kila mmoja Alhamisi na kuwawezesha Atletico kupata ushindi wa jumla wa 8-1.

Atletico wameshinda Europa League mara mbili na walifika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili 2014 na 2016 – walishindwa mara zote mbili.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Danny Welbeck (mawili) na Granit Xhaka naye Hakan Calhanoglu akawafungia Milan bao la kufutia machozi Alhamisi.

“Bila shaka tungependa kuwakwepa Atletico Madrid,” alisema Wenger.

Hata hivyo, alisema hana usemi wowote na wakikabidhiwa klabu hiyo hawatakuwa na budi ila kukutana nao.

Droo ya robofainali – ambapo kuna klabu nane kutoka mataifa manane – itafanyika leo Ijumaa saa 12:00 GMT.

Huu ulikuwa ushindi wa tatu wa Arsenal katika kipindi cha wiki moja baada ya kuwalaza Milan 2-0 mechi ya kwanza mjini Milan na pia wakalza Watford 3-0 Ligi ya Premia Jumapili.

Lakini kabla ya ushindi huo San Siro, walikuwa wameshindwa mechi nne mtawalia mashindano yote – mara mbili ikiwa mikononi mwa Manchester City.

“Mambo ni mazuri sana leo. Tulihitaji kujikwamua kutoka kwa matokeo yetu,” Wenger alisema.

“Inaonesha jinsi timu ilivyochukua hatua. Tulikuwa na mechi ngumu lakini mwishowe tulishinda. Tukiwa na matokeo mazuri na jinsi tunavyocheza soka, mashabiki watatuunga mkono.”

“Ilikuwa mechi wazi. Tulicheza kwa kurejesha mpira nyuma mara nyingi zaidi kipindi cha kwanza kujilinda na kujaribu kutetea matokeo ya mechi ya kwanza. Tulicheza dhidi ya timu nzuri sana,” alisema Wenger.

“Ni lazima tujiimarishe katika safu ya ulinzi, lakini kwa jumla yetu ni timu yenye ustadi kiufundi ambayo zaidi huangazia kushambulia.

“Huwa twatatizika zaidi wakati tunahitajika kujilinda. Tulimaliza mechi hiyo tukiwa imara zaidi.”

 

https://youtu.be/pwdeOcOezmM