WATU 17 wametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara kwa tuhuma za kujihusisha na makosa mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Issa Suleiman – SACP amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo mauaji, kulawiti, kupatikana na pombe haramu ya moshi (Gongo) na mengine.

“Watuhumiwa hao yamekamatwa kufuatia operesheni na misako iliyofanyika  katika maeneo mbalimbali kuanzia Novemba 01,2024 hadi Desemba 12 mwaka huu,”amesema Suleiman.

Baadhi ya watuhumiwa wa matukio hayo wakiwemo 5 ambao wamekamatwa na dawa hizo zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya aina ya bangi kilo 22 na watuhumiwa 7 wakiwa na lita 160 za pombe haramu aina ya gongo,

Pia mitambo miwili ya kutengenezea pombe hiyo na pikipiki moja aina ya Haojue yenye  usajii wa Mc 772 BUS waliyokuwa wakitumia kusafirisha pombe hiyo na tayari wameshafikiwa mahakamani kesi zao zopo katika hatua mbalimbali.

Watuhumiwa 2 wamekamatwa katika benki ya NMB wilayani Nanyumbu wakiwa na noti bandia 20 na kila noti moja ikiwa na thamani ya dola mia moja za kimarekani na upekelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Hata hivyo watumiwa wengine 3 akiwemo Juma Said (44) mkazi kijiji cha chilolo wilayani Masasi amehukumiwa kifungo cha maisha jela katika mahakama ya Wilaya ya Masasi kwa kosa la kubaka Aprili 30, 2024 kijijini hapo baada ya kimvizia mtoto wa kike mwenye umri wa miaka (06) mwanafunzi wa chekechea akiwa amelala yake jikoni.

Mwingine ni Swedy Yusufu (19) mkazi wa kijiji cha Mkachima wilayani humo amehukumiwa kifungo cha maisha jela mahakamani hapo kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza na alitenda kosa hilo Januari 1, mwaka huu katika kambi ya tohara ya mkachima akiwa kama mwangalizi wa watoto waliyofanyiwa tohara kambini hapo.

Nae Mwalimu wa shule ya msingi Namalembo wilayani humo, Mponda Ambari (32) amehukumiwa kifungo cha maika 30 jela  mahakamani hapo kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita (16) Oktoba 10 mwaka huu kwenye nyumba za shuleni hapo baada ya kumlaghai kwa kumpatia pesa ndogo ndogo za matumizi na kuahidi kuwa atamuowa.

“Jeshi la polisi halitasita kuwatafuta, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wananchi hususani wale wote wanaofanya uhalifu kisha kukimbia katika maeneo wanayoishi kwa kuwepo mkono wa sheria