Maandishi ya historia za watu wengi maarufu yanajikita kuelezea maisha yao ya kawaida lakini maisha kama tunavyoyafahamu yana mambo mengi sana, hata hao watu maarufu wana visa na vituko vingi ambavyo ni nadra sana kuonekana katika maandiko kuhusu maisha yao.

UNSPECIFIED – MAY 28: Charles Dickens (1812-1870) english novelist, 1860’s (Photo by Apic/Getty Images)

Mambo ni hivyo hivyo kwa Charles Dickens, mmoja wa watunzi maarufu wa vitabu wa zamani nchini Uingereza.

Lakini pamoja na kuandika vitabu maarufu kama ‘A Tale of Two Cities’, ‘Oliver Twist’ na hadithi ya kutisha ya ‘A Christmas Carol’, Dickens pia alikuwa mtu wa vituko vya ajabu.

Wakati ambapo Dickens alikuwa haandiki vitabu, alipenda kuwafanyia watu wengine mzaha sana. Mathalani, angeweza kuwakuta watu wanazungumza na yeye akaanza kuzungumza kwa lugha ambayo ameibuni, ambayo haipo, akijifanya naye kushiriki kwenye mazungumzo hayo.

Hilo liliwaacha wengi vinywa wazi kwa sababu hakuna aliyekuwa anaelewa anazungumza kitu gani.

Wakati mwingine angeweza kuwa anatembea mtaani halafu akamsimamisha mtu na kujifanya anamuuliza jambo fulani huku akizungumza kwa ishara na miguno isiyoeleweka na kuwaacha watu wakimshangaa.

Katika moja ya vituko vyake, siku moja alikuwa anakwenda kwenye ufukwe wa bahari akamkamata mwanamke mmoja, akamburuza mpaka kwenye ukingo wa maji na kutishia kumuua.

Alimwambia mwanamke huyo kuwa yeye (Dickens) anampenda na angetaka wafe pamoja hivyo amepanga kumuingiza kwenye maji mengi ili wafe wote. 

Wakati akiyasema hayo alikuwa anaonyesha kama mtu ambaye amedhamiria kweli kulifanya jambo hilo. Ebu fikiria woga ambao mwanamke huyo ulimpata! Kumbe Dickens alikuwa anafanya mzaha tu!

Historia ya Dicken inaonyesha kuwa ingawa hakuwahi kwenda shule maalumu, lakini alifanya kazi ya uhariri kwa miaka 20, akaandika vitabu vya riwaya 15, michezo ya kuigiza mitano, mamia ya hadithi fupifupi na habari nyingi magazetini. Pia alikuwa mhadhiri na mwanaharakati wa kudai haki za watoto.

Dickens alizaliwa Februari 7, 1812 Portsmouth, Uingereza na kufariki dunia Juni 9, 1870.

Lakini kabla ya kufikia hatua hiyo, kutokana na umaskini wa familia yake, Dickens aliacha shule na kulazimika kufanya kazi baada ya mwili wa baba yake kuchomwa moto gerezani na mtu ambaye alikuwa anamdai.